Kinunggubuyu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kinunggubuyu ni lugha ya Kigunwinyguan nchini Australia inayozungumzwa na Wanunggubuyu katika jimbo la Northern Territory. Katika sensa ya mwaka 2006, idadi ya wasemaji wa Kinunggubuyu ilihesabiwa kuwa watu 110 tu, yaani lugha iko hatarini mwa kutoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kinunggubuyu kiko katika kundi la Kiarnhem cha Mashariki pamoja na Kingandi na Kianindilyakwa.