Kingandi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kingandi ni lugha ya Kigunwinyguan nchini Australia inayozungumzwa na Wangandi katika jimbo la Northern Territory. Katika sensa ya mwaka 2006, idadi ya wasemaji wa Kingandi ilihesabiwa kuwa watu tisa tu, yaani lugha iko hatarini mwa kutoweka. Mwaka wa 2017, msemaji mzee wa mwisho wa kuweza kutumia Kingandi kihodari akaanza kuwafundisha Wangandi wa vizazi vya kisasa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kingandi kiko katika kundi la Kiarnhem cha Mashariki pamoja na Kinunggubuyu na Kianindilyakwa.