King'amuzi rada (pia: Ditekta ya rada kutoka jina "Radar Detector" kwa lugha ya Kiingereza) ni kifaa cha teknolojia ya juu kinachotambua iwapo mwendo wa gari unafwatiliwa na polisi au walinda sheria wakitumia tochi ya kutambua mwendo (radar gun).

Thumb
King'amuzi Rada
Thumb
Ditekta ya zamani kidogo.
Thumb
Ditekta ya Kijapani.

Kifaa hicho cha umeme hutumiwa sanasana na dereva wa gari kuchunguza kama kasi ya magari yao inatazamwa kwa kutumia bunduki ya rada na askari wa usalama wa barabarani au maofisa wengine wa usalama. Wakitambua maeneo ambayo maafisa wa kudhibiti mwendo walipo wanapunguza kasi ya gari kabla ya kusimamishwa na kupewa faini au kutiwa mashakani.

Sheria

Hata hivyo umiliki na matumizi ya King'amuzi rada ni kinyume cha sheria katika nchi nyingi duniani na huchukuliwa kama uvunjaji sheria. Chombo hiki ni kinyume cha sheria kwenye nchi kama vile Australia, Ubelgiji, Brazili na Ufaransa, wakati katika nchi za Japani, Kazakistani, Pakistani na Ufilipino ni halali.

Marekani ni mojawapo kati ya nchi ambako ni kinyume cha sheria kutumia king'amuzi rada bila leseni maalum.[1] Katika baadhi ya nchi, polisi hutumia ditekta ya ditekta ya rada ili kutambua madereva wanaotumia chombo hiki.

Kutumia au kuwa na ditekta ya rada ni kinyume cha sheria katika nchi mbalimbali ambapo ukikutwa nacho unaadhibiwa kwa faini na kunyang'anywa chombo hiki. Nchi hizi huamini kuwa madereva wanaotumia chombo hivi wanahatarisha maisha ya watumiaji wa barabara kuliko madereva wasiotumia.

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.