![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/4/48/Pel%2527s_Anomalure.jpg/640px-Pel%2527s_Anomalure.jpg&w=640&q=50)
Kindi Mrukaji
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kindi warukaji ni wanyama wadogo hadi wakubwa kiasi wa familia Anomaluridae. Wanatokea misitu ya Afrika kusini kwa Sahara. Kuna kindi warukaji huko Asia pia, lakini jamii hizi hazina mnasaba. Wale wa Afrika wana ngozi kati ya miguu ya mbele na ya nyuma, isipokuwa spishi moja, kindi mkia-magamba. Upande wa chini wa msingo wa mkia wao mrefu una mistari miwili ya magamba yenye ncha kali yanayomsaidia mnyama ili kupanda juu ya miti. Rangi yao ni kijivu, kahawia, kahawiachekundu au hudhurungi. Hula matunda, makokwa, maua na majani na pengine wadudu pia.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Kindi mrukaji | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Kindi mrukaji wa Pel (Anomalurus pelii) | ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Jenasi 3, spishi 7:
| ||||||||||||
Funga