Kimasana
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kimasana ni lugha ya Kiafrika-Kiasia nchini Chad na Kamerun inayozungumzwa na Wamasana. Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kimasana nchini Chad imehesabiwa kuwa watu 130,000 na mwaka wa 1982 nchini Kamerun imehesabiwa kuwa watu 103,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimasana iko katika kundi la Kichadiki.