Kimalta
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kimalta ni lugha rasmi kwenye nchi ya kisiwani ya Malta katikati ya Bahari ya Mediteranea. Kimalta huhesabiwa kati ya lugha za Kisemiti ikiwa ni lugha pekee ya familia hiyo katika nchi za Ulaya.
Kimalta ni karibu na Kiarabu cha Tunisia lakini huandikwa kwa alfabeti ya Kilatini. Misingi ya sarufi ni Kiarabu, lakini lugha imepokea maneno mengi kutoka Kiitalia na Kiingereza. Siku hizi takriban nusu ya maneno yana asili ya Kiitalia, na theluthi moja ni Kiarabu. Mengine yameingia kutoka Kiingereza.