Kilahu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kilahu ni lugha ya Kisino-Tibeti nchini Uchina, Myanmar, Laos, Vietnam na Uthai inayozungumzwa na Walahu. Mwaka wa 2007 idadi ya wasemaji wa Kilahu imehesabiwa kuwa watu 280,000 nchini Uchina. Pia kuna wasemaji 200,000 nchini Myanmar (2012), 32,000 nchini Uthai (2001), 8700 nchini Laos (1995) na 9650 nchini Vietnam (2009). Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kilahu iko katika kundi la Kingwi.