Kikungkari
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kikungkari kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wakungkari katika jimbo la Queensland. Isichanganywe na lugha ya Kikunggari. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kikungkari ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikungkari kiko katika kundi la Kikarniki.