Kigupapuyngu
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kigupapuyngu ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wagupapuyngu katika jimbo la Northern Territory. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kigupapuyngu 330. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kigupapuyngu kiko katika kundi la Kiyolngu. Wengine hukiangalia kuwa Lahaja ya Kidhuwal.