Kigundungurra
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kigundungurra kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wagundungurra katika jimbo la New South Wales. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea Kigundungurra, yaani lugha imetoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kigundungurra kiko katika kundi la Kiyuin. Wengine hukiangalia kuwa lahaja ya Kingunawal.