Kingunawal
lugha ya asili ya Australia iliyotoweka / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kingunawal kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wangunawal katika jimbo la New South Wales. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea Kingunawal, yaani lugha imetoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kingunawal kiko katika kundi la Kiyuin.