![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/4/44/Bunaban_languages.png/640px-Bunaban_languages.png&w=640&q=50)
Kigooniyandi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kigooniyandi (au Kiguniyandi) ni lugha ya asili nchini Australia inayozungumzwa na Wagooniyandi katika jimbo la Australia ya Magharibi. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kigooniyandi 410 tu, wote watu wazima, yaani lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kigooniyandi inahusiana na lugha Kibunaba tu, yaani hizo mbili ziko katika familia ya lugha peke yake.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/4/44/Bunaban_languages.png/640px-Bunaban_languages.png)