Kigiyug
lugha ya asili ya Australia iliyotoweka / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kigiyug kilikuwa lugha ya Kidaly nchini Australia iliyozungumzwa na Wagiyug katika jimbo la Northern Territory. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea Kigiyug, yaani lugha imetoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kigiyug kiko katika kundi la Kiwagaydy lakini wengine husema kwamba hakihusiani na lugha nyingine yoyote.