Kigithabul
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kigithabul ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wagithabul katika jimbo la Australia ya Magharibi. Mwaka wa 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kigithabul ishirini tu, yaani lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kigithabul kiko katika kundi la Kibandjalangiki. Wengine hukiangalia kama lahaja ya Kibandjalang.