Kidadi-Dadi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kidadi-Dadi ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wadadi-Dadi mpakani katikati ya majimbo ya Victoria na New South Wales. Mwaka wa 2005, kulikuwa na wasemaji wa Kidadi-Dadi kumi tu, yaani lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kidadi-Dadi kiko katika kundi la Kimurray cha Chini. Wengine hukiangalia kama lahaja ya Kiyitha-Yitha.