Kimandarini
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kimandarini ni lugha ya Kisino-Tibeti nchini Uchina inayozungumzwa na Wachina. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kimandarini nchini Uchina imehesabiwa kuwa watu milioni 840. Pia kuna wasemaji katika nchi zifuatazo: 24,320,000 nchini Taiwan (1993), 10,600 nchini Brunei (2006), 60,900 ndani ya Hong Kong (2006), 460,000 nchini Indonesia (1982), wengi nchini Malaysia ambapo ni lugha ya taifa (lakini bila idadi rasmi ya wasemaji), 35,000 nchini Mongolia (1993), 500,000 nchini Myanmar (1994), 500 nchini Ufilipino (1990), 1,210,000 nchini Singapuri (2010), na 5,880 nchini Uthai (1984). Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kimandarini iko katika kundi la Kichina.