Kibatyala
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kibatyala ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wabatyala katika jimbo la Queensland. Mwaka wa 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kibatyala saba tu, yaani lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibatyala kiko katika kundi la Kiwaka-Kabiki. Wengine huiangalia kama lahaja ya Kigabi-Gabi.