Kiarakwal
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiarakwal ilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Waarakwal katika jimbo la New South Wales. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kiarakwal ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiarakwal kiko katika kundi la Kibandjalang.