Kaunti ya Kiambu
Kaunti ya Kenya / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kaunti ya Kiambu ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.
- Kuhusu mji, soma Kiambu
Ukweli wa haraka Nchi, Ilianzishwa ...
Kaunti ya Kiambu | |||
---|---|---|---|
Kaunti | |||
| |||
Kiambu County in Kenya.svg Kaunti ya Kiambu katika Kenya | |||
Nchi | Kenya | ||
Ilianzishwa | Machi 4th 2013 | ||
Ilitanguliwa na | Mkoa wa Kati | ||
Makao Makuu | Kiambu | ||
Gavana | Ferdinand Waititu | ||
Naibu wa Gavana | Dkt. James Nyoro | ||
Seneta | Kimani Wamatangi | ||
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa) | Gathoni wa Muchomba | ||
Bunge la Kaunti | Bunge la Kaunti ya Kiambu | ||
Spika | Stephen Ndichu[1] | ||
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa | 60[2] | ||
Maeneo bunge/Kaunti ndogo | 12 | ||
Eneo | km2 2 538.6 (sq mi 980.2) | ||
Idadi ya watu | 2,417,735 | ||
Wiani wa idadi ya watu | 952 | ||
Kanda muda | Saa za Afrika Mashariki (UTC+3) | ||
Tovuti | kiambu.go.ke |
Funga
Ilikuwa mojawapo ya wilaya za Kenya katika Mkoa wa Kati baada ya nchi kupata uhuru.
Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 2,417,735 katika eneo la km2 2,538.6, msongamano ukiwa hivyo wa watu 952 kwa kilometa mraba[3].
Kupakana na Nairobi kumeifanya iwe na idadi ya wakazi wengi mijini, kwa sababu ya maendeleo katika sekta ya mali yasiyohamishika. Sekta za viwanda na ukulima pia zimechangia kukuza kaunti hii kiuchumi.
Makao makuu ya kaunti hii ni mji wa Kiambu. Hata hivyo, utendaji wa kaunti hutekeleza majukumu yake kutoka Thika, ambayo wilaya yake imemezwa tena na Kiambu (2010).