Kanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli (pia Imani ya Nikea) ni fomula rasmi ambayo ilipitishwa na Mtaguso wa kwanza wa Nisea (325)[1] ikakamilishwa na Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli (381) ili kubainisha imani sahihi ya Kanisa Katoliki dhidi ya uzushi, hasa wa Ario na wafuasi wake.
Katima mazingira hayo, lengo kuu lilikuwa kwanza kumkiri Yesu kama Mungu kweli sawa na Baba, halafu kwamba Roho Mtakatifu anastahili kuabudiwa pamoja na Baba na Mwana (Utatu Mtakatifu).
Hadi leo hiyo kanuni ya imani inatumika sana katika madhehebu mengi ya Ukristo, hata kama sehemu ya liturujia.[2][3][4][5][6][7][8][9]