![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/6/61/East_African_Springhare_%2528Pedetes_surdaster%2529_%25288290878677%2529.jpg/640px-East_African_Springhare_%2528Pedetes_surdaster%2529_%25288290878677%2529.jpg&w=640&q=50)
Kamendegere
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kamendegere ni wanyama wakubwa kiasi wa jenasi Pedetes, jenasi pekee wa familia Pedetidae, ambao wanafanana na sungura wenye miguu ya nyuma mirefu au hata na kanguru mdogo, lakini hawana mnasaba na wanyama hawa. Rangi yao ni hudhurungi juu na nyeupe chini. Wanatokea nyika za Afrika ya Kusini na ya Mashariki[1][2]. Hukiakia usiku; wakati wa mchana hupumzika katika matundu yao ambayo wayachimba wenyewe. Hula mimea, mizizi na pengine wadudu. Jike huzaa mwaka mzima, mtoto mmoja kwa mara na mara tatu kwa mwaka.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Kamendegere | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Kamendegere mashariki (Pedetes surdaster) | ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Spishi 2:
| ||||||||||||||
Funga