![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/1/1b/Anton_von_Maron_006.png/640px-Anton_von_Maron_006.png&w=640&q=50)
Kaizari Joseph II
ukarasa wa maana wa Wikimedia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Joseph II (13 Machi 1741 ā 20 Februari 1790) alikuwa Kaizari wa Dola la Ujerumani kuanzia 1765 hadi kifo chake. Alimfuata baba yake, Francis I, na kufuatwa na mdogo wake, Leopold II.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/1/1b/Anton_von_Maron_006.png/640px-Anton_von_Maron_006.png)
Sera zake katika utawala Austria peke yake miaka 1780-1790 zimeitwa Ujosefu (au Josefini). Sera hizo zilifuata falsafa ya mwangaza na kuingilia na kubana mamlaka ya Kanisa katika mambo mengi, hata madogo sana.
Kwa sababu hiyo alilaumiwa vikali na Kanisa Katoliki na kuhusianishwa na tapo la Wamasoni.
Pamoja na hilo, alipatwa na upinzani mkubwa, na hatimaye alifuta baadhi ya maamuzi yake.
Alipokufa, Leopoldo II alizidi kurudisha mambo yalivyokuwa awali na kujali hisia za wananchi.