From Wikipedia, the free encyclopedia
Maji ya matunda (au sharubati kwa neno lenye asili ya Kiarabu; pia: juisi kwa neno la mkopo kutoka Kiingereza "juice" ambalo lilitokana na maneno ya Kifaransa cha Kale "jus, juis, jouis" yaliyomaanisha maji yanayopatikana kwa kuchemsha mimea ya dawa.[1]) ni kinywaji kinachotokana na matunda ya mimea na mboga kinachotengenezwa kwa kusindika matunda ya aina moja au mchanganyiko wa matunda mengi au mboga.
Kuna aina nyingi sana za sharubati, sawa na wingi wa matunda yanayolika. Hasa matunda yenye majimaji mengi ndani yake yanafaa kwa kutengeneza maji ya matunda.
Watu wengi hupenda kunywa sharubati, kwa mfano ya
na mengine mengi.
Pamoja na utamu wake, kinywaji kama hicho kinafaa sana kwa afya, kwa sababu kinaongeza haraka vitamini muhimu mwilini. Kwa mfano, sharubati ya chungwa yenye vitamini C, asidi ya foliki, na potasiamu,[2].
Haya hivyo, unywaji wa kiasi cha juu wa maji ya matunda yaliyoongezwa sukari kunaweza kusababisha kuongezeka kwa uzito wa mwili [3][4] ingawa sio tafiti zote zinaonyesha athari hii [5]. Maji ya matunda yakitokana na asilimia 100 na matunda, binadamu hupata viwango vya virutubisho vinavyohitajiwa kwa siku.If 100% from fruit, juice can help meet daily intake recommendations for some nutrients.[6]
Kama tunda lina asidi nyingi kiasi ndani yake sukari huongezwa, lakini matunda mengine, hasa kama ni mabivu na yameiva penye jua kali, huwa na sukari ya kutosha ndani yake.
Katika nchi nyingi maji ya matunda hutengenezwa kiwandani na kuuzwa madukani. Watu wengi wanajua na wanapenda zaidi kujitengenezea nyumbani kwa kutumia mashine ya kukamua matunda.
Nchi inayoongoza kwa kuwa na watu wengi wanaokunywa maji ya matunda ni New Zealand ikifuatiwa na Kolombia.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.