John Glenn
From Wikipedia, the free encyclopedia
John Herschel Glenn Jr (18 Julai 1921 ā 8 Desemba 2016) alikuwa mwanaanga na mwanasiasa kutoka nchini Marekani.
Anajulikana sana kwa kuwa Mmarekani wa kwanza kuzunguka Dunia kwenye mwaka 1962 kama mwanaanga NASA. Baada ya kazi yake kama mwanaanga, aliingia kwenye siasa na aliwahi kuwa Seneta kutoka jimbo lake la Ohio miaka 1974-1999.
Mnamo 1998, alirushwa kwenye anga-nje mara ya pili akiwa na umri wa miaka 77, akijitolea kwa utafiti kuhusu athira ya hali isiyo na graviti kwa wazee. Yeye ndiye mtu wa zamani zaidi katika anga za juu. [1]