From Wikipedia, the free encyclopedia
Jiwe mchanga (kwa Kiingereza: sandstone) ni aina ya mwamba mashapo. Linaundwa na mchanga uliogandamizwa, hivyo madini ndani yake ni hasa shondo na felispa.
Jiwe mchanga ni mwamba thabiti ambayo hailikwi kirahisi, pia si ngumu mno, hivyo hutumiwa kwa ujenzi katika nchi nyingi.
Jiwe mchanga linabadilika kuwa kwasiti kama inaathiriwa na shinikizo kubwa, kwa mfano chini ya matabaka ya ardhi au kama linalala chini ya milima.
Jiwe mchanga huundwa katika hatua mbili. Kwanza, mchanga unakaa na kuunda tabaka la mashapo.
Baada ya matabaka ya mashapo mapya zaidi hukusanya juu yake, hili tabaka la mashapo linagandamizwa na uzito wa matabaka ya juu yakiimarishwa kuwa jiwe.
Oksidi ya chuma mara nyingi hufanya jiwe mchanga liwe na rangi nyekundu.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.