Jina la kuzaliwa
From Wikipedia, the free encyclopedia
Jina la kuzaliwa (kwa Kiingereza: birth name, full name, legal name au en:Personal name) ni kundi la majina ambalo kwa pamoja linamtambulisha mtu maalumu. Katika tamaduni kadhaa ni majina mawili, katika nyingine ni matatu, ambapo la kwanza ni la mwenyewe, la pili la baba, la tatu la babu au la ukoo[1]. Tamaduni chache zinatumia jina moja tu au zaidi ya tatu.