James Omingo Magara
From Wikipedia, the free encyclopedia
James Omingo Magara ni mwanasiasa wa Kenya. Kwa sasa ni mwanachama wa Orange Democratic Movement na alichaguliwa kuwa mbunge wa Mugirango Kusini katika uchaguzi wa 2007.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/sw/a/a2/Jamesomingomagara.jpg)
Alishinda kiti hiki mara ya kwanza kwa tiketi ya FORD-Kenya katika uchaguzi mdogo mnamo 2001, akichukua nafasi ya nduguye Enock Nyakieya Magara aliyefariki katika ajali ya gari.
Alihifadhi kiti chake katika Uchaguzi mkuu wa Kenya wa 2002, wakati huu akiwakilisha chama cha Ford People na pia katika Uchaguzi wa 2007, akiwakilisha Chama cha ODM[1]