Jamaika
From Wikipedia, the free encyclopedia
Jamaika ni nchi ya kisiwani katika Bahari ya Karibi. Iko km 150 kusini mwa Kuba na 150 upande wa magharibi wa Haiti na ni kisiwa kikubwa cha tatu kati ya Antili Kubwa. Katika lugha ya Kiingereza visiwa hivyo huitwa "West Indies" (visiwa vya Uhindi wa Magharibi).
Ukweli wa haraka
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Out of many, one people (kutoka wengi - taifa moja) | |||||
Wimbo wa taifa: Jamaica, Land We Love Wimbo wa kifalme: God Save the King | |||||
Mji mkuu | Kingston 17°59′ N 76°48′ W | ||||
Mji mkubwa nchini | Kingston | ||||
Lugha rasmi | Kiingereza | ||||
Serikali Mkuu wa Dola (Mfalme) Gavana Mkuu Waziri Mkuu |
Ufalme wa kikatiba Charles III Sir Patrick Allen Andrew Holness | ||||
Uhuru kutoka Uingereza |
6 Agosti 1962 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
10,991 km² (ya 166) 1.5 | ||||
Idadi ya watu - Julai 2012 kadirio - Msongamano wa watu |
2,889,187 (ya 139) 252/km² (ya 49) | ||||
Fedha | Dollar ya Jamaika (JMD ) | ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC-5) (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .jm | ||||
Kodi ya simu | +1-876]]
- |
Funga
Jina limetokana na neno la Kiarawak "Xaymaca" au "Chaymaka" linalomaanisha "nchi ya chemchemi" (yaani kisiwa chenye maji matamu).