Ila Arun
Mwanamuziki na Muigizaji wa India / From Wikipedia, the free encyclopedia
Ila Arun (alizaliwa Jodhpur, jimbo la Rajasthan, India, mnamo 15 Machi 1952) ni mwigizaji wa filamu za Kihindi, mtangazaji katika televisheni, mwimbaji, Mwimbaji wa ufatilizi ambaye anafahamikaa kwa kazi zake katika sinema za Kihindi.[1] Ameonekana katika sinema nyingi maarufu za Bollywood kama vile Lamhe, Jodhaa Akbar, Shaadi Ke Side Effects na Begum Jaan.
Ila Arun | |
---|---|
| |
Jina la kuzaliwa | Ila Arun |
Alizaliwa | 15-03-1952 |
Nchi | India |
Kazi yake | Mwigizaji, Muimbaji na Mtangazaji |
Ndoa | Arun Bajpai |
Watoto | Ishita Arun |
Ila Arun ni mwimbaji anayependwa sana, mwigizaji anayejulikana na mwenye mvuto katika runinga. Alihitimu kutoka Chuo cha Wasichana cha Maharani huko Jaipur. Ila Arun anasifika kwa sauti yake nzuri na ya kuvutia na talanta ya kushangaza aliyonayo. Alianza kuonekana kwenye runninga kwa mara ya kwanza kwenye kipindi cha Televisheni cha kihindi cha Lifeline (Jeevanrekha), ambacho kilisisitiza maisha ya kawaida ya madaktari kilichokuwa kikirushwa kupitia stesheni ya Doordarshan.[2]