Milango ya fahamu ni ogani za mwili zinazoturuhusu kujua mazingira yetu. Mifano yake ni macho na masikio. Ni njia asili ya kutambua mtazamo au hisia.
Kibiolojia inaelezwa kuwa ogani yenye uwezo wa kupokea habari za nje ya mwili, kama vile nuru, sauti, halijoto, mwendo, harufu au ladha, na kuzibadilisha katika mishtuko ya umeme inayofikishwa kwa njia ya mfumo wa neva hadi ubongo.
Kama milango ya fahamu imeharibika, tunasema mtu ni kipofu, bubu au kiziwi, ana matatizo kuelewa mazingira yake sawa na jinsi wanavyoweza watu wengine.
Milango ya fahamu ni muhimu sana kwa Viumbe hai kutokana na kwamba inasadia kiumbe hai katika shughuli zake za kila siku, hasa katika kufatuta mahitaji muhimu (kwa Kiingereza yanaitwa Basic needs).
Fahamu zetu
Mara nyingi watu hutaja fahamu tano([1] [2]) ambazo ni:
- Kusikia ni fahamu ya sauti kupitia masikio
- Kuona ni fahamu ya nuru kupitia macho
- Kuonja ni fahamu ya ladha kupitia ulimi
- Kunusa ni fahamu ya harufu kupitia pua
- Mguso ni fahamu ya nyuso za vitu kupitia ngozi, hasa ya mkono
Hali halisi kuna fahamu zaidi:
Mfumo wa kibiolojia ya fahamu zetu
Ogani mbalimbali za mwili ziko tayari kupokea vichocheo kutoka mazingira yetu.
Neva katika ogani husika zina uwezo wa kupokea vichocheo vya nje vinavyotafsiriwa katika ubongo kwa fahamu mbalimbali
- vichocheo vya kikemia vinavyotuwezesha kuonja na kunusa[3]
- vichocheo vya nuru vinavyotuwezesha kuona[4]
- vichocheo vya halijoto vinavyotuwezesha kutofautisha joto na baridi[5]
- vichocheo vya shinikizo na mwendo[6]
- vichocheo vya athari hatari vinavyotafsiriwa na ubongo kwa maumivu au kichefuchefu[7]
Wanyama pia wana ogani zinazowawezesha kutambua:
- vichocheo vya kusumaku (kwa mfano ndege wanaohamahama mbali kila mwaka kwa kufuata uga wa sumaku wa dunia)
- vichocheo vya umeme
- vichocheo vya mnururisho sumakuumeme nje ya nuru ya kawaida, kwa mfano nyuki hutambua mawimbi ya urujuanimno yasiyoonekana na binadamu
Picha za milango ya fahamu
- Jicho la nzi
- Muundo wa sikio
- Pua kubwa halinusi kushinda pua dogo!
- Ngozi ni mlango wa fahamu mbalimbali
- Ulimi
Marejeo
Wikiwand in your browser!
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.