Herman wa Alaska
From Wikipedia, the free encyclopedia
Herman wa Alaska (kwa Kirusi Преподобный Герман Аляскинский, Prepodobnyy German Alyaskinskiy; Serpukhov au Voronezh Governorate, Russia, 1750 hivi – Spruce Island, 15 Novemba 1836) alikuwa mmonaki wa Kanisa la Kiorthodoksi la Urusi aliyefanya umisionari huko Alaska, leo jimbo la Marekani.
Tarehe 9 Agosti 1970 alitangazwa na Waorthodoksi kuwa mtakatifu na inatumika kwa sikukuu yake ya kila mwaka.