Hendrick Witbooi
Shujaa wa kitaifa wa Namibia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Hendrick Witbooi, kwa jina asilia ǃNanseb ǀGabemab (1840 - 1905) alikuwa chifu wa kabila la Nama katika Namibia ya leo, kiongozi wa mapambano dhidi ya ukoloni wa Kijerumani na mwandishi.
Alizaliwa katika jimbo la rasi la Afrika Kusini akalelewa kama Mkristo. Mnamo 1855 alihamia pamoja na kabila lote Namibia. Alikuwa mtoto wa chifu wa awali akapokea uongozi kutoka kwa baba.
Katika miaka ya 1880 aliunganisha makabila yote ya Wanama chini ya uongozi wake na tangu 1890 aliingia katika mapambano na wakoloni Wajerumani. Baada ya kushondwa mara ya kwanza alipatana amani lakini wakati wa vita ya Wajerumani dhidi ya Waherero alijiunga nao. Mwaka wa 1905 alikamatwa na kuuawa na Wajerumani.
Shajara yake aliyoiandika kwa lugha ya Kiholanzi ilitolewa mwaka wa 1929 tu.