![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/5/51/Haematopus_ostralegus_He.jpg/640px-Haematopus_ostralegus_He.jpg&w=640&q=50)
Kizamiachaza
From Wikipedia, the free encyclopedia
Vizamiachaza ni ndege wa jenasi Haematopus, jenasi pekee ya familia Haematopodidae. Ndege hawa ni weusi au weusi na weupe na wana domo na macho nyekundu na miguu pinki au myeupe. Huonekana pwani kwa kawaida ambapo hutafuta chakula wakiingiza domo lao kwa matope. Hula wanyamakombe, mwata, nyungunyungu na lava wa wadudu, pengine wanyama ngozi-miiba, kaa na samaki pia. Ndege wanaokula wanyamakombe wana domo lenye ncha nyembamba kama ubapa na hulitumia kulifungua kombe ikikata musuli wa mnyama. Wale wanaokula nyungunyungu wana domo kama msharasi. Hii ni kwa sababu ya uchakavu. Vizamiachaza hutaga mayai 2-4 chini ndani ya tundu ya kina kifupi.
Kizamiachaza | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Kizamiachaza wa Ulaya | ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||