Gumawesi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Gumawesi (kwa Kiingereza: basalt) ni mwamba wa mgando wenye rangi nyeusi-nyeusi.
Imetokana na lava kiowevu iliyotoka kwenye volkeno na kupoa haraka. Gumawesi ni mwamba mgumu unaoweza kudumu muda mrefu.
Mawe ya gumawesi hutumiwa katika ujenzi wa barabara ama katika tabaka la kokoto chini ya uso wa njia au kama vibapa vinavyofanya uso wa njia. Karibu na volkeno za zamani penye gumawesi tele hutumiwa pia kwa ujenzi wa nyumba na vijiji au miji katika mazingira hayo huwa na nyumba nyeusi.
Aina maalumu ya gumawesi huyeyushwa kiwandani kwa joto kali na kupata umbo la nyuzi zinazotumiwa kufuma mikeka ya kuzuia moto katika utengenezaji wa magari au eropleni. Ni nyuzi mbadala kwa asbesto bila kuwa hatari kwa afya.