![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/d/d4/Gabriel_Martinelli_2020.jpg/640px-Gabriel_Martinelli_2020.jpg&w=640&q=50)
Gabriel Martinelli
Mcheza mpira wa Brazil / From Wikipedia, the free encyclopedia
Gabriel Teodoro Martinelli Silva (anajulikana kama Gabriel Martinelli, alizaliwa 18 Juni 2001 [1]) ni mchezaji wa soka wa nchini Brazil ambaye anacheza kama mshambuliaji katika klabu ya Ligi kuu Uingereza Arsenal FC na timu ya taifa ya Brazil.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/d/d4/Gabriel_Martinelli_2020.jpg/640px-Gabriel_Martinelli_2020.jpg)
Martinelli alizaliwa na kukulia huko Guarulhos, alianza kucheza soka la kulipwa katika klabu ya wakubwa akiichezea timu ya Ituano na akasajiliwa na Arsenal Julai 2019, akiwa na umri wa miaka 18. Alishinda Kombe la FA katika mechi yake ya kwanza kama mchezaji wa Arsenal.