Funguvisiwa la Franz Josef
From Wikipedia, the free encyclopedia
Funguvisiwa la Franz Josef au Nchi ya Franz Josef (au Funguvisiwa/Nchi ya Frants Iosif) ni funguvisiwa upande wa kaskazini wa Novaya Zemlya katika Bahari Aktiki. Ni sehemu ya Urusi na kuhesabiwa kama sehemu ya mkoa wa Arkhangelsk Oblast. Ni kundi la visiwa 191.
Ni eneo baridi sana. Usafiri wa kuondoka unapatikana kwenye wiki chache cha majirajoto pekee. Sehemu ya karibu zaidi ya Urusi bara ni umbali wa kilomita 750, umbali na Novaya Zemlya ni km 370.
Sehemu ya kaskazini kabisa ya visiwa iko kwenye umbali wa kilomita 900 pekee kutoka ncha ya kaskazini, kwa hiyo ni karibu pia na Greenland na Kisiwa cha Ellesmere cha Kanada.
Visiwa hivyo 191 vina eneo kwa jumla la kilomita za mraba 16,134 na vinasambaa katika eneo lenye upana wa kilomita 375 kutoka Mashariki kwenda Magharibi na kilomita 234 kwa kutazama kusini - kaskazini.
Mwaka 2007 kulikuwa na wakazi 9 pekee, wanne wao wako kwenye kituo cha jiografia cha Kisiwa cha Hayes na watu watano wanaoangalia hali ya hewa kwenye kituo cha Nagurskoye kwenye kisiwa cha Alexandra.