Filipo wa Yesu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Filipo wa Yesu (1572 - 1597) alikuwa bradha wa shirika la Ndugu Wadogo Pekupeku kutoka Meksiko na mmisionari aliyefia dini Japani .
Dhuluma dhidi ya Wakatoliki zilipozidi, yeye na wenzake 25 (mapadri na watawa 8 na walei 17[1]) walikamatwa, walitukanwa na kuteswa vikali, na hatimaye wakasulubiwa huko Nagasaki tarehe 5 Februari mwaka 1597, huku wakifurahia neema ya kuuawa namna ileile ya Yesu.
Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake na ya wafiadini wenzake huadhimishwa kila mwaka tarehe 6 Februari[2].