Fahrenheit
From Wikipedia, the free encyclopedia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Fahrenheit (kikamilifu vizio vya fahrenheit) ni kipimo cha halijoto. Alama yake ni °F.
Skeli ya fahrenheit ilibuniwa 1724 na mwanafizikia Mjerumani Daniel Gabriel Fahrenheit. Ilikuwa skeli ya kupima halijoto iliyotumiwa sana duniani lakini wakati wa karne ya 20 skeli ya selsiasi ilichukua nafasi yake kwa sababu inalingana na vipimo sanifu vya kimataifa. Leo hii fahrenheit hutumiwa hasa Marekani na nchi chache nyingine kama Belize.
Kwenye skeli ya fahrenheit kiwango cha kuganda kwa maji ni 32 °F na kiwango cha kuchemka kwa maji ni 212 °F. Kwa hiyo kuna vizio 180 kati ya halijoto ya maji kuganda na kuchemka. Sifuri ya fahrenheit inalingana na −17,8 °C kwenye skeli ya selsiasi.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.