Everest (mlima)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mlima Everest ni mlima mkubwa kabisa duniani, wenye kimo cha m 8,848 juu ya usawa wa bahari. Ni sehemu ya safu ya milima ya Himalaya.
Kilele chake kipo katika mpaka wa Nepal na China (Tibet).
Watu wa kwanza wa kufika kwenye kilele walikuwa Edmund Hillary wa New Zealand na sherpa Tenzing Norgay wa Nepal tarehe 29 Mei 1953.