From Wikipedia, the free encyclopedia
Escopetarra ni gitaa iliyotengeneza na bunduki inayotumika kama ishara ya amani. Jina limeundwa kutokana na maneno mawili Kihispania escopeta (bunduki) na guitarra (gitaa).[1]
Escopetarra ilibuniwa na mwanaharakati wa Kolombia César López kwenye mwaka 2003[2]. Kiasili alitengeneza nakala tano alizokabidhi kwa rafiki zake waliokuwa wanamuziki Juanes na Fito Páez, halafu Mradi wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) na Jiji la Bogota. Nakala moja aliyobaki nayo aliuza baadaye kwa $ 17,000 kwenye mkutano wa kuchangia pesa kwa wahanga wa mabomu ya ardhini[3].
Nakala ya escopetarra iliyopewa kwa UNDP ilionyeshwa kenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu upunguzaji wa silaha za vita duniani[4]. Baadaye imeonyeshwa hadharani katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.