Punda ni wanyama wakubwa kiasi wa nusujenasi Asinus ya jenasi Equus katika familia Equidae wafananao na farasi mdogo. Spishi moja (Equus kiang), ambayo inatokea Asia, huitwa kiang'. Punda anayejulikana sana ni yule anayefugwa (Punda-kaya), lakini kuna punda porini pia. Watu huwatumia punda wafugwao kwa kubeba mizigo, kuvuta magari au kuwarakibu. Punda wanaweza kuzaliana na farasi lakini watoto wao (baghala au nyumbu) hawazai tena kwa kawaida.
Punda | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Punda-kaya katika Hifadhi ya Taifa ya Amboseli | ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Spishi 3, nususpishi 12:
| ||||||||||||||
Spishi
- Equus africanus, Punda wa Afrika (African Wild Ass)[1][2]
- Equus a. africanus, Punda Nubi (Nubian Wild Ass)
- †Equus a. atlanticus, Punda Kaskazi Atlas Wild Ass – imekwisha sasa
- Equus a. somalicus, Punda Somali Somali Wild Ass)
- Equus asinus, Punda-kaya (Donkey)
- Equus hemionus, Punda wa Asia (Onager au Asiatic Ass)
- Equus h. hemionus, Punda wa Mongolia (Mongolian Wild Ass, Khulan au Kulan)
- †Equus h. hemippus, Punda wa Syria (Syrian Wild Ass) – imekwisha sasa
- Equus h. khur, Punda wa Uhindi (Indian Wild Ass au Khur)
- Equus h. kulan, Punda wa Turkmenistan (Turkmenian Kulan)[3]
- Equus h. onager, Punda wa Uajemi (Persian onager)
- Equus kiang, Kiang' (Kiang)
- Equus k. chu, Kiang' Kaskazi (Northern Kiang)
- Equus k. holdereri, Kiang' Mashariki (Eastern Kiang)
- Equus k. kiang, Kiang' Magharibi (Western Kiang)
- Equus k. polyodon, Kiang' Kusi (Southern Kiang)
Spishi za kabla ya historia
- †Equus calobatus, Punda Miguu-mirefu (Stilt-legged Onager)
- †Equus cumminsii, Punda wa Cummin (Cummin’s Ass)
- †Equus francisci au Equus tau, Punda Kibete (Pygmy Onager)
- †Equus hydruntinus, Punda wa Ulaya (European Ass)
- †Equus lambei, Punda wa Yukon (Yukon Wild Ass)
Picha
- Punda Nubi
- Punda Somali
- Punda wa Mongolia
- Punda wa Uhindi
- Punda wa Turkmenistan
- Punda wa Uajemi
- Kiang' mashariki
Marejeo
Wikiwand in your browser!
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.