Edirne
From Wikipedia, the free encyclopedia
Edirne (anc. Hadrianopolis; Kigiriki Adrianòpolis, Αδριανουπολις; Kibulgaria Одрин ni mji katika sehemu ya magharibi mwa nchi ya Uturuki, katika sehemu yake iliyopo kwenye bara la Ulaya, karibu kabisa na mipaka ya Ugiriki na Bulgaria. Huu ni mji mkuu wa Jimbo la Edirne una wakazi wapatao 128,400, kwa mwaka wa 2002 kutoka lundiko la watu kiasi cha 119,298 cha mwaka wa 2000.