Dondoo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Dondoo | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Dondoo-nyika (Raphicerus campestris) | ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Spishi 3:
| ||||||||||||||||
Funga
Dondoo, dondoro au isha ni wanyamapori wadogo wa jenasi Raphicerus katika familia Bovidae wenye masikio makubwa. Wana rangi ya mchanga inayoelekea nyekundu na mara nyingi madoa au milima nyeupe. Madume wana pembe fupi na laini. Wanatokea Afrika ya Kusini na ya Mashariki katika maeneo mbalimbali kutoka ukanda wa jangwa mpaka vilima vyenye msitu wazi. Wanyama hawa hula majani, vitawi, mizizi na viazi.