Donati wa Arezzo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Donati wa Arezzo (alifariki Arezzo, Toscana, Italia, 7 Agosti 362 BK) anakumbukwa kama askofu wa 2 wa mji huo wa Italia ya Kati. Labda alitokea Nikomedia, leo nchini Uturuki, au Roma.
Papa Gregori I alimsifu kwa maadili na kwa uwezo wa sala yake[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu, pengine kama mfiadini pia.