Denizli ni mji uliopo mwishoni mwa mashariki ya mto Büyük Menderes, ambapo kuna maporomoko ya mita zaidi ya mia, katika kusini-magharibi mwa nchi ya Uturuki, kwenye Mkoa wa Aegean.

Thumb
Ukumbi wa manispaa ya mji wa Denizli.

Mji una wakazi wapatao 400,000 (kwa sensa ya 2006) na ndiyo mji mkuu wa Jimbo la Denizli katika Majimbo ya Uturuki. Huu ni mji unaokua sana katika sekta ya viwanda.

Mji wa Denizli umepata mafanikio makubwa sana kiuchumi hasa kwa shughuli zake za utengenezaji wa nguo na kuzusafirisha nchi za nje[1].

Mji huu umekuwa kituo kikubwa cha uzalishaji wa bidhaa zinazotazamiwa kupelekwa nchi za nje, Denizli hutajwa mara kwa mara, ukiwa sambamba na miji mingine ya Uturuki, ikiwa kama miji yenye kupiga hatu kubwa sana kimaendeleo[2].

Jina

Jina la Denizli linamaana ya "maeneo yenye bahari au ziwa" kwa Kituruki, lakini mji wenyewe haupo katika pwani. Jina linatokana na tahajia kadha wa kadha ambazo zina vyanzo vya maji yanayopita chini kwa chini na kuelekea katika eneo la mkoa wa karibu ya ziwa lililopo karibu na mji huko Uturuki.[3]

Historia

Watu mashuhuri

  • Ahmet Nazif Zorlu - Mfanyabiashara
  • Sezen Aksu - Mwimbaji wa Pop
  • Bayram Şit - Mwanamiereka aliyepokea nishani ya Olimpiki
  • Cem Bahtiyar - Mpiga basi-gitaa wa kundi la muziki wa rock la maNga
  • Hasan Güngör - Mwanamiereka aliyepokea nishani ya Olympic
  • Nezih Altın - Mwnafizikia mashuhuri (kwa sasa anaishi mjini Adıyaman)
  • Özay Gönlüm - Mwimbaji nyimbo za asili (1940-2000)
  • Rıza Esendemir DJ bora wa redio FM ya Istanbul
  • Sarp - Mwimbaji wa rock

Marejeo

Viungo vya nje

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.