From Wikipedia, the free encyclopedia
Idadi ya wakazi wa Afrika imeongezeka sana katika karne ya mwisho,[1] na kwa sababu hiyo wengi wao ni watoto na vijana, pia kwa sababu matarajio ya kuishi si ya miaka mingi (katika nchi nne ni chini ya miaka 50).[2]
Katika miaka 1982–2009 idadi ya watu imekuwa maradufu[3] tena ukihesabu miaka 1955–2009 imekuwa mara nne zaidi.[4]
Kwa sasa ongezeko ni la asilimia 2.6 kwa mwaka na wakazi wa Afrika wamekuwa 1,225,080,510 (2016), sawa na 15% za watu wote duniani. Umoja wa Mataifa unatabiri kwamba wanaweza kufikia 26% mwaka 2050 (2,500,000,000) na 39% mwaka 2100 (4,400,000,000).[5]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.