Kekeo ni ndege wadogo hadi wakubwa kiasi wa nusufamilia Cuculinae katika familia Cuculidae. Wana mkia mrefu na mabawa marefu na membamba. Miguu yao ina vidole viwili vikabilivyo mbele na viwili vikabilivyo nyuma. Rangi zao kuu ni nyeusi, nyeupe na rangi ya kijivi, pengine rangi ya majani na ya manjano. Kekeo hula wadudu, mabuu ya wadudu na matunda, na spishi kubwa hula wanyama wadogo pia.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Kekeo |
Kekeo kidari-chekundu |
Uainishaji wa kisayansi |
Himaya: |
Animalia (Wanyama)
|
Faila: |
Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
|
Ngeli: |
Aves (Ndege)
|
Oda: |
Cuculiformes (Ndege kama kekeo)
|
Familia: |
Cuculidae (Ndege walio na mnasaba na kekeo)
|
Nusufamilia: |
Cuculinae (Ndege wanaofanana na kekeo)
|
|
Ngazi za chini |
Jenasi 12:
- Cacomantis Muller, 1843
- Cercococcyx Cabanis, 1882
- Chrysococcyx Boie, 1826
- Clamator Kaup, 1829
- Cuculus Linnaeus, 1758
- Eudynamys Vigors & Horsfield, 1827
- Hierococcyx Müller, 1845
- Microdynamis Salvadori, 1878
- Pachycoccyx Cabanis, 1882
- Scythrops Latham, 1790
- Surniculus Lesson, 1830
- Urodynamis Salvadori, 1880
|
Funga
Kekeo hawajengi tago lao lenyewe lakini hutaga mayai yao katika matago ya ndege wengine, yai moja katika kila tago baada ya kutoa yai moja la mwenye tago (udusio wa kiota, Kiing. brood parasitism). Kwa kawaida mayai ya kekeo yafanana na yale ya mwenye tago. Mara nyingi ndani ya domo la makinda yao ni sawasawa na ile ya makinda ya mwenyewe, pengine wanafanana kabisa, lakini kinda la kekeo ni takriban kila mara mkubwa zaidi. Akitoka yai ayasukuma mayai au makinda ya mwenyewe nje ya tago. Mwenye tago aendelea kumpa kinda la kekeo chakula.
- Cercococcyx mechowi, Kekeo Mkia-mrefu Kijivucheusi (Dusky Long-tailed Cuckoo)
- Cercococcyx montanus, Kekeo Mkia-mrefu Miraba (Barred Long-tailed Cuckoo)
- Cercococcyx olivinus, Kekeo Mkia-mrefu Zeituni (Olive Long-tailed Cuckoo)
- Chrysococcyx caprius, Kekeo Didariki (Dideric Cuckoo)
- Chrysococcyx cupreus, Kekeo Kijani (African Emerald Cuckoo)
- Chrysococcyx flavigularis, Kekeo Koo-njano (Yellow-throated Cuckoo)
- Chrysococcyx klaas, Kekeo Shaba (Klaas's Cuckoo)
- Clamator glandarius, Kekeo Madoa (Great Spotted Cuckoo)
- Clamator jacobinus, Kekeo Rangi-mbili (Jacobin au Pied Cuckoo) – pengine inaainishwa ndani ya jenasi Oxylophus
- Clamator levaillantii, Kekeo Michirizi-myeusi (Levaillant's Cuckoo) – pengine inaainishwa ndani ya jenasi Oxylophus
- Cuculus canorus, Kekeo wa Ulaya (Common Cuckoo)
- Cuculus clamosus, Kekeo Mweusi (Black Cuckoo)
- Cuculus gularis, Kekeo Kijivu (African Cuckoo)
- Cuculus poliocephalus, Kekeo Mdogo (Lesser Cuckoo)
- Cuculus rochii, Kekeo wa Madagaska (Madagascar Cuckoo)
- Cuculus solitarius, Kekeo Kidari-chekundu (Red-chested Cuckoo)
- Nannococcyx psix, Kekeo Mdogo wa Saint Helena (Saint Helena Cuckoo) imekwisha sasa (karne ya 18)
- Pachycoccyx audeberti, Kekeo Domo-nene (Thick-billed Cuckoo)
- Eocuculus sp. - (Mwisho wa Eocene ya Teller County, MMA)
- Eudynamis cf. taitensis (Henderson Island Koel) (Mwisho wa Quaternary)
Kekeo didariki
Kekeo kijani
Kekeo shaba
Kekeo madoa
Kekeo rangi-mbili
Kekeo michirizi-myeusi
Kekeo wa Ulaya
Kekeo mweusi
Kekeo kijivu
Kekeo mdogo
Kekeo wa Madagaska
Kekeo kidari-chekundu
Kekeo domo-nene
Moluccan cuckoo
Chestnut-breasted cuckoo
Fan-tailed cuckoo
Plaintive cuckoo
Pallid cuckoo
Grey-bellied cuckoo
Rusty-breasted cuckoo
Banded bay cuckoo
Brush cuckoo
Horsfield's bronze cuckoo
Shining bronze cuckoo
Asian emerald cuckoo
Long-billed cuckoo
White-eared bronze cuckoo
Little bronze cuckoo
Black-eared cuckoo
Gould's bronze cuckoo
Violet cuckoo
Chestnut-winged cuckoo
Sunda cuckoo
Indian cuckoo
Himalayan cuckoo
Oriental cuckoo
Pacific koel
Asian koel
Dark hawk-cuckoo
Malaysian hawk-cuckoo
Rufous hawk-cuckoo
Hodgson's hawk-cuckoo
Philippine hawk-cuckoo
Large hawk-cuckoo
Moustached hawk-cuckoo
Common hawk-cuckoo
Channel-billed cuckoo
Fork-tailed drongo-cuckoo
Square-tailed drongo-cuckoo
Philippine drongo-cuckoo