Cleveland Browns
From Wikipedia, the free encyclopedia
Cleveland Browns ni timu ya kitaalam ya football iliyoko Cleveland, Ohio, nchini Marekani. Wanashindana kwenye Ligi ya Football ya Kitaifa (NFL) na wamepewa jina la mkufunzi na mwanzilishi wao wa kwanza, Paul Brown.[1]
Timu ya Browns hucheza michezo yao ya nyumbani kwenye Uwanja wa First Energy[2] na ofisi zao za ushirika ziko Barea, Ohio, kitongoji cha Cleveland.[3] Rangi rasmi ya Browns ni kahawia, machungwa, na nyeupe. Ndio timu pekee kwenye Ligi ya Football ya Kitaifa ambayo haina nembo kwenye helmeti zao.[4][5]
Wameshinda mashindano manne ya Shirikisho la Football la Amerika (AAFC) na manne ya NFL, lakini hawajawahi kushinda au kwenda Super Bowl, ambayo iliundwa baada ya ushindi wa mwisho wa Browns mwaka 1964.[6] Watu kumi na sita ambao walichezea Browns wameingizwa kwenye Jumba la Umaarufu la Football. Jim Brown, Running Back ambaye alichezea Browns kutoka 1957-1965, anachukuliwa na wanahistoria wengi wa football kuwa mchezaji bora wa mpira wa miguu wakati wote.[7]