Ciudad de la Paz
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ciudad de la Paz (Kihispania: Mji wa Amani), [1] zamani iliitwa Oyala, ni mji katika Guinea ya Ikweta ambao unaendelea kujengwa kwenye mwaka 2022. Inakusudiwa kuchukua nafasi ya Malabo kama mji mkuu wa taifa. [2] [3]
Ilianzishwa kama eneo la mjini wa mkoa Wele-Nzas kwenye mwaka wa 2015.[4] Sasa ni makao makuu ya utawala ya mkoa mpya wa Djibloho ulioundwa mwaka wa 2017.[5] Mnamo 2017, mji huo ulipewa jina rasmi la Ciudad de la Paz ("Mji wa Amani"). [6] [7]
Mahali pa mji mpya palichaguliwa kwa ufikiaji wake mzuri na tabianchi. Kusudi muhimu ilikuwa kuunda mji mkuu kwenye eneo la bara, tofauti na mji mkuu wa sasa Malabo, ambao uko kwenye kisiwa cha Bioko .
Mji ulipangwa na kampuni ya usanifu ya Ureno. Unakusudiwa kuwa na takriban wakazi 200,000, [8] jengo jipya la bunge, ikulu ya rais na eneo la hekta 8150.
Ujenzi wa mji mkuu huu mpya umekosolewa na wapinzani wa kisiasa kwa Rais Teodoro Obiang aliyesukuma mpango huo. Serikali ya Guinea ya Ikweta ilianza kuhamia ofisi za kwanza tangu mwaka wa 2017. [9]