From Wikipedia, the free encyclopedia
Popo ni mamalia kama panya wenye mabawa.
Popo | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Popo-masikio wa Townsend (Corynorhinus townsendii) | ||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Nusuoda 2:
| ||||||||||
Spishi zake nyingi sana hula wadudu: hizi zimo katika nusuoda Yangochiroptera.
Spishi kubwa za nusuoda hii hula ndege, mijusi, vyura na hata samaki.
Spishi chache za popo wanyonya-damu huko Amerika ya Kusini hula damu ya mamalia au ndege.
Familia Pteropodidae ya nusuoda Yinpterochiroptera ina spishi kubwa hadi ukubwa wa paka na uzito wa kilogramu moja; urefu wa mabawa pamoja unaweza kufikia sentimita 150. Spishi hizi hula matunda.
Hapo awali, popo waligawanywa katika nusuoda Microchiroptera na Megachiroptera. Walakini, tafiti za ADN zilifunua kuwa baadhi ya familia za Microchiroptera zilikuwa karibu na Megachiroptera. Kwa hivyo, nusuoda mbili mpya zilipendekezwa, Yangochiroptera na Yinpterochiroptera. Nusuoda ya mwisho imegawanywa katika familia za juu Pteropodoidea (popo-matunda) na Rhinolophoidea (popo-wadudu; spishi mbalimbali hula vertebrata wadogo).
Popo wengi hutumia sauti kwa kutambua mazingira yao, yaani wanatumia mwangwi wa mlio wao kukadiria umbali hadi kizuizi au hata windo pamoja na ukubwa na maumbile ya vitu vilivyopo njiani. Kwa hiyo masikio yao ni mlango wa fahamu muhimu zaidi. Kinyume chake popo wengi hawana macho mazima ingawa hakuna aliye kipofu kabisa. Lakini kuna pia aina nyingine wanaoona vizuri sana.
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Popo kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.